Viongozi zaidi ya 35 wahutubia, ulinzi wa amani wamulikwa, soka yachezwa… Pata taarifa zote kuhusu yaliyojiri leo.

  • Hotuba rasmi

Leo ilikuwa ni siku ya kwanza ya kikao cha ngazi ya juu cha baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mjadala wa wazi ukifunguliwa rasmi na hotuba ya Katibu Mkuu Antònio Guterres. Katibu Mkuu hakutafuna maneno akianza kwa kutamka wazi kwamba dunia imeathirika na ugonjwa wa ukosefu wa uaminifu. Dawa ni moja tu, ameongeza: ushirikiano wa kimataifa. Soma zaidi.

Naye Rais wa Baraza Kuu María Fernanda Espinosa amewasihi viongozi wa dunia kudumisha umoja, na kufanya kazi pamoja katika juhudi za kuelekea utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu.

Rais wa Baraza Kuu Bi Espinoza akikaa na Naibu Katibu Mkuu Amina Mohamed (kushoto)

 

Miongoni mwa marais waliohutubia leo ni Rais Paul Kagame ambaye amesisitiza mafanikio yaliyopatikana katika Muungano wa Afrika, ambao aliongoza mwaka huu. Ametaja kutiwa saini kwa eneo la biashara huru Afrika (CFTA) na kuboresha matumizi ya fedha ya shirika hilo, pamoja wa kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa katika masuala ya ulinzi wa amani.

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa upande wake amehakikisha kwamba uchaguzi wa rais utafanyika mwaka huu kwa nija ya amani na uwazi.

Timu ya video ikifuatilia hotuba ya rais Donald Trump.

  • Ulinzi wa amani

Nchi 145 zimeunga mkono mkakati mpya wa Umoja wa Mataifa unaolenga kuimarisha mfumo wa ulinzi wa amani, kupitia:

  • kuimarisha usalama wa walinda amani,
  • kuongeza uwiano wa wanawake walinda amani
  • kushirikisha zaidi mashirika kama vila Muungano wa Afrika.

Picha ya UN Peacekeeping

 

  • Soka yachezwa na wasichana

Leo pia, timu mbali mbali za watetezi wa Malengo Endelevu wamekusanyika mjini New York kwa ajili ya kucheza mpira wa miguu. Refarii alikuwa ni mwigizaji Nikolaj Caster-Waldau ambaye anajulikana kama Jaime Lannister kwenye filamu ya Game of Thrones.

 

  • Yatakayojiri jumatano kwenye #UNGA

Mjadala wa wazi wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa utaendelea na hotuba za marais na mawaziri wakiwemo wa Uganda na Kenya. Usikose kuzifuatilia mbashara hapa.

Jumatano pia ni siku ya kimataifa dhidi ya majaribio ya silaha za nyuklia. Zaidi ya majaribio 2,000 ya nyuklia yameshatekelezwa kote duniani, amesema Katibu Mkuu katika ujumbe wake kwa siku hiyo akieleza kwamba matukio hayo yameathiri zaidi watu wanaoishi kwenye mazingira magumu zaidi.

 

Maelezo mengine hapa