Maadhimisho ya miaka mia ya Mandela, uzinduzi wa mkakati kwa vijana, waimbaji kutoka Korea…   Mikutano ya ngazi ya juu iliyofanyika leo Jumatatu tarehe 24, Septemba imemulika changamoto za kimataifa.

Maandalizi yalianza na mazungumzo baina ya Katibu Mkuu Antònio Guterres na mwandishi wa habari wa Al-Jazeera Femi Oke, yakiwa mbashara kwenye mtandao wa Facebook. Katibu Mkuu alijibu maswali yaliyoulizwa na raia kutoka sehemu mbalimbali duniani, akitaja nchi za Afrika kama mfano kwa nchi tajiri.

 

Picha ya selfi iliyochukuliwa na Femi Oke na Antònio Guterres kabla ya mahojiano yake.

 

  • Rais Trump ataka dunia bila madawa ya kulevya

Rais wa Marekani Donald Trump aliongoza kikao cha kwanza cha siku hiyo kuhusu tatizo la madawa ya kulevya akiahidi kuwa “Marekani inatarajia kufanya kazi na wote ili kujenga mustakhabali bila madawa ya kulevya kwa watoto wetu wote”. Watu 450,000 wanafariki dunia kila mwaka kwa sababu ya madhara ya madawa ya kulevya. Katibu Mkuu Antònio Guterres amesema ni jukumu letu kuchukua hatua kwa tatizo hilo linalotuhusu sote.

Rais wa Marekani Donald Trump na Katibu Mkuu Antònio Guterres.

  • Sanamu ya Mandela yawekwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa

Leo pia ilikuwa ni maadhimisho ya miaka mia ya kuzaliwa kwa Hayati Nelson Mandela. Sanamu yake ya kuchonga ikazinduliwa kwenye makao makuu hapa jijini New York. Wakati wa hafla maalumu ya uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema, “leo twamkumbuka mtu mwenye hekima, heshima na ufanisi mkubwa zaidi, ambaye alifanya kazi kwa bidii kwa ajili ya amani na heshima kwa binadamu wote ulimwenguni. Mandela alikuwa ni mtu ni mwenye kuiga maadili ya juu ya Umoja wa Mataifa – amani, msamaha, huruma na utu kwa binadamu. Alikuwa ni bingwa kwa watu wote – kwa maneno yake na kwa vitendo vyake”. Soma zaidi

  • Vijana wachangamsha ukumbi kwa ajili ya #Youth2030

Macho yote yakaangazia upande wa New York wakati ambapo kundi la waimbaji kutoka Korea BTS wakashiriki katika uzinduzi wa mkakati mpya wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya vijana.

High Level Event on Youth2030 to launch the United Nations Strategy and the Generation Unlimited Partnership
BTS at the United Nations listening to the SG speak and speaking themselves.

Katibu Mkuu akasema lazima tupaze sauti za vijana na tuwape fursa za uongozi. Kwa sababu wao ndio wanaomiliki suluhu za changamoto zinazoikumba dunia. Soma zaidi.

  • Mkuu wa UNCTAD aeleza faida za uhamiaji – kwa Kiswahili!

Katika studio yetu maalum ya mitandao ya kijamii, tuliwapokea viongozi wengi, akiwemo Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD. Akiongea na Flora Nducha wa idhaa ya Kiswahili, Dkt. Kituyi amesema kuuchukulia uhamiaji kama tatizo si fikra nzuri, kwani uhamiaji una faida nyingi, kwa wahamiaji wenyewe lakini pia kwa jamii zinazowahifadhi, iwe katika masuala ya kiuchumi, utamaduni na hata maendeleo. Soma zaidi na angalia video yake.

Mukhisa Kituyi (kulia) akihojiwa na Flora Nducha.

  • Kitakachojiri Jumanne kwenye Umoja wa Mataifa

Jumanne tarehe 25 Septemba ni mwanzo wa hotuba za viongozi wote wa dunia. Tayari marais 35 wamepangwa kuhutubia Baraza Kuu siku hiyo. Unaweza kupata orodha kamili hapa.

Maelezo mengine hapa