Jumatatu hii tarehe 24, Septemba ni mwanzo wa wiki ya mjadala wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa. Viongozi wengi, marais na mawaziri, idadi yao ikiwa kubwa zaidi kulilo miaka iliyopita, wanatarajiwa kuhudhuria mikutano hii. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antònio Guterres amewahimiza kuhuisha ushirikiano wa kimataifa, wakati ambapo changamoto za kimataifa zinaathiri ushirikiano huo.

  • Mandela Peace Summit

Jumatatu mkutano wa kwanza utakuwa ni Kongamano la Amani la Mandela, likiwa ni katika maadhimisho ya miaka mia ya kuzaliwa kwake. Shiriki kwenye mazungumzo kwa kutumia hashtag #Mandela100 na fuatilia tukio mbashara hapa.

Kongamano la Amani la Mandela

 

  • #Youth2030

Uzinduzi wa mkakati mpya kwa vijana, #Youth2030 ni moja ya matukio muhimu ya wiki hii. Kundi la wanamuziki vijana BTS na mtu mashuhuri kwenye Youtube Lily Singh watahudhuria mkutano huo. Fuatilia mbashara kwenye Youtube na Snapchat pia! Angalia GIFs nzuri tulizotengeneza hapa.

#youth2030 ni mkakati ulioundwa na vijana na kwa ajili yao.

 

  • Financing for Development 

Hatimaye usikose kujiunga na mazungumzo kuhusu ufadhili wa Malengo Endelevu yaani Global Goals wakati wa mkutano wa ngazi ya juu unaoitishwa na Katibu Mkuu. Hashtag itakuwa ni #Fin4Dev

Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu ufadhili wa maendeleo.

Maelezo mengine hapa