Kila mwezi Septemba, viongozi wa dunia na watu mashuhuri ulimwenguni hukusanyika jijini New York kwa ajili ya “Kikao cha Baraza Kuu” la Umoja wa Mataifa(UM). Vile vile, kuna vikao vingi vya ngazi ya juu, vikao maalum na vikao vya pembeni vinavyoendelea kwenye makao makuu na maeneo mbalimbali jijini humo.

Idara ya Habari ya Umoja wa Mataifa imejizatiti kuwakaribisha watu kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni kwenye vikao hivi kupitia mitandao maalum. Kikao hiki cha kimataifa pia kina alama yake maalum ya reli pamoja na Emoji.

Hizi ndizo njia 7 ambazo unaweza kushiriki katika kongamano la kimataifa.

1. Tumia alama maalum ya reli – #UNGA

Mamilioni ya watu ulimwenguni kote wamejiandikisha kupata yanayojiri kutoka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za UM na mamilioni na zaidi ya watu wanazungumzia mada zinazohusu UM. Unaweza kushiriki katika mijadala hii kwa kupitia alama maalumu ya reli ya #UNGA katika kurasa zako za mitandao ya kijamii. Alama hii imeambatanishwa na alama maalumu ya Emoji ya UM, shukrani kwa uwezeshaji kutoka Twitter.

2. Fuata ukurasa wa Umoja wa Mataifa wa Facebook

Tizama video mubashara kupitia Facebook, inaburudisha, njia shirikishi ya kukuunganisha na UM. Vivyohivyo, katika ukurasa wa Facebook wa Umoja wa Mataifa tutasambaza matukio muhimu ya siku, maonesho ya picha na zaidi

3. Tweet na @UmojaWaMataifa kwenye Twitter

Kufuata @UmojaWaMataifa kwenye Twitter ni njia bora zaidi ya kupata taarifa mpya zinazojiri kila wakati, nukuu, picha za yanayojiri nyuma ya pazia pamoja na kazi zingine za midia-anuai.

4. Fuatilia mbashara kwenye TV mtandaoni

Vikao kamili vya #UNGA, mikutano ya ngazi za juu, mikutano muhimu na mikutano ya pembeni itaoneshwa mubashara kupitia http://webtv.un.org.  Hakikisha unakuwa nasi wiki nzima. Unataka kujua nani anazungumza lini? Tizama mpangilio kamili

5. Angalia yanayojiri kwenye Instagram na Flickr

Pata picha ya yanayojiri kutoka kwa wafanyakazi wanaoshiriki kwenye mikutano kwa kufuata @um_kiswahili kwenye Instagram.  Picha katika galleria ya Flickr zitawekwa kadri matukio yanavyotokea.

6. Tuma maswali yako

Matukio mengine yatahitaji wewe kutuma maswali na maudhui. Fursa hizi zitatangazwa kwenye Twitter kupitia ukurasa wa @UmojaWaMataifa

7. Ungana na Umoja wa Mataifa kupitia lugha mbalimbali na katika jukwaa nyinginezo

Kwa fursa zingine za kujihusisha na UM kupitia lugha unayopenda na kujifunza na kufahamu zaidi shughuli zinazoendelea ulimwenguni, hakikisha unafuatilia kurasa zetu zingine kama LinkedIn, Weibo, Tumblr, Google+ na zaidi.

Shukran kwa kushiriki! Usisite kutujuza unachofikiri! Timu yetu — kama ilivyo hapo juu  — itafurahi kupokea mrejesho wako kuhusu habari tutakazokuletea. Unaweza kuwasiliana nasi kupitia socialmedia@un.org.