Unatarajia kuhudhuria mikutano ya #UNGA? Angalia jinsi ya kujipatia kitambulisho maalum yaani ID card.

Ufunguzi wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kinatarajiwa kufanyika tarehe 18, Septemba, 2018. Sasa ni wakati kwa washiriki wa mikutano hii kutoka kwa nchi mbalimbali duniani kutafuta vitambulisho vyao ili kuweza kuruhusiwa kuingia ndani ya
jengo la Umoja wa Mataifa na kwenye vyumba vya mikutano.

Waandishi wa habari, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na waalikwa wengine wanatakiwa kupitia kwanza ofisi ya vitambulisho ya UN iliyoko 320 East 45th Street karibu ya jengo la Umoja wa Mataifa. Wawakilishi wa NGOs wataweza kupata vitambulisho vyao kwa mikutano maalum kwenye ofisiiliyoko katika 2nd avenue na 46th Street.

Pata maelezo zaidi.