Je ungependa kusambaza mada zinazohusu Kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mitandaoni? Hapa utapata taarifa zaidi za jinsi Timu yetu ya Mitandao ya Kijamii inavyoweza kukusaidia.

Kwa mara nyingine, wakati wa kikao cha mwaka huu ambao utafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani katikati mwa mwezi Septemba, tutakuwa na Studio Maalumu ya Mitandao ya Kijamii. Viongozi wa ulimwengu, watu mashuhuri pamoja na wadau wengine kutoka asasi za kiraia wamealikwa kurekodi ujumbe wao maalumu kwa ajili ya mashabiki na wafuasi uliwenguni kote.

Tunashukuru Facebook, Instagram, Twitter na Snapchat kwa kutusaidia kutafuta mbinu bunifu za kuonyesha shughuli zetu mitandaoni.